CONGREGATION MELECH YISRAEL OF TORONTO
Usharika wa Melech Yisrael, Toronto, Canada - Kehilat Melech Yisrael, A Messianic Jewish Torah Observant Congregation, in Toronto, Canada / קהילת מלך ישראל, קהילה משיחית יהודית שומרת בתורה, הנימצאה בטורונתו, קנדה

פרשות השבוע - Parashot HaShavua

 Masomo ya Biblia Kwenye Mtandao

ENGLISH / ESPAÑOL / PORTUGUÊS / ITALIANO / FRANÇAIS / MAGYAR / KISWAHILI / / 한국어 / РУССКИЙ / עברית

Masomo ya wiki hii

YHome
YMonthly News Letters
YServices & Special Activities
YLocation Map
YWho we Are
YMission Statement
YWhat is Messianic Judaism?
YCMY Academy Day School
YBooks of Life Catalogue
YRebbetzin Corner
YLinks
..

Y Our E mail
Y Our ICQ Is # 79381635

.

  Jiunge na kundi la email
  

Masihi Myahudi

* DO WE WANT MASHIACH NOW?
FALSE MESSIAHS - TRUE MESSIAH
DO YOU WANT MASHIACH NOW?

UNTIL MASHIACH RETURNS

מתשובה למשיח לגאולה במהרה בימינו. זכריה י"ב:י'
ברוך הבא מלך המשיח!

אני מאמין באמונה שלמה בביאת המשיח ואף על פי שיתמהמה עם כל זה אחכה לו בכל יום שיבוא.

Radio Melech HaMashiach - רדיו מלך המשיח; a Messianic Jewish Radio Station on the Internet.

ישועה וגאולה אמיתית לכל ישראל.

פרשת השבוע צו
Parashat Tzav / Amuru

Y Vayikra / Walawi 6:1-8:36
Y Yermiyahu / Yer. 7:21-8:3, 9:22-23
Y Messianic Jews / Ebrania 8:1-6
Y
Kuwasha Mishumaa 7:30  p.m.
Y Mwisho wa Shabati  8:43 p.m.
Y Kutoa Nakala safi (Bonyeza)
Y שבת הגדול / Shabbat HaGadol
Y Kuchangia huduma (Bonyeza)

פרשת השבוע צו / Prashati HaShavua Tzav / Amuru; Usharika wa Melech Yisrael, Toronto, Canada
Shiur 5766
5765 Shiur / Masomo (
Bonyeza)

"Sote Twahitaji Korban, Sote Twahitaji 'Kusogea Karibu'"

 

Parashat Tzav / Amri

Orodha ya Masomo ya wiki hii:

Y Vayikra / Walawi 6:1-8:36

Y Yeshayahu / Isaya 43:21- 44:23

Y Ivrim / Waibrania 10:1-18

 

Vayikra / Walawi  {6:20} Tangu wakati wa kuwekwa wakfu kwa Aharoni (Aroni) na wazawa wake wanapaswa kumtolea HaShem: kikumi cha efah moja ya unga laini kwa siku, nusu moja ya unga huo atautoa asubuhi na nusu nyingine jioni. {6:21} Unga huo utachanganywa na mafuta na kuokwa juu ya karai; kisha utauleta ukiwa vipandevipande na kumtolea HaShem dhabihu ya hiari yenye harufu nzuri yakupendeza mbele Zake. {6:22} Kuhani aliye mzawa wa Aharoni ambaye amepakwa mafuta kushika nafasi yake atamtolea HaShem sadaka hiyo; hilo ni agizo la milele. Sadaka yote itateketezwa kwa HaShem. {6:23} Kila dhabihu ya hiari itakayotolewa na kuhani itateketezwa yote; haitaliwa kamwe.

HaShem hana ustahiki na mwanadamu kama inavyoonyesha katika kifungu hiki cha Parasha Tzav. Aharoni na familia yake, japo kuwa walikuwa na wadhifa wa juu kama familia Kuu ya Kikuhani, bado walikuwa ni wanadamu tu na hivyo kuisimu katika dhambi zilezile na majaribu ambayo sote tunakumbana nayo. Matokeo yake ni kwamba, wao pia iliwabidi kutoa korbanot (dhabihu za kusogea karibu) kwa HaShem kabla ya kuhudumu mbele Zake.

Inanisikitisha ninaposikia mara kwa mara kuhusu marabbi, wachungaji na mapadri wanaojiinua juu ya watu katika sharika zao. Wanajiona wao wako katika kiwango tofauti, kilicho juu, na kutarajia washirika wao wawatumikie. Nimesikia viongozi wa sharika wakitarajia sharika zao kuwanunulia magari ya gharama, kuwaruzuku na majumba ya kifahari kama vile wao ni wafalme, wakijiweka wao kuwa ni makuhani wakuu wa sharika zao.

Basi, kufuatana na Parasha yetu ya wiki hii, famila hii ya Makuhani Wakuu, ingawa walikuwa na shughuli maalumu ya muhimu mbele za M-ngu, bado walihitaji kutoa korban kabla hata hawajamsogelea Yeye.

Bila shaka Yisraeli (Israeli) walihitaji kuheshimu wadhifa wa Kohen HaGadoli (Kuhani Mkuu), lakini hiyo haikumaanisha kwamba alikuwa na kiwango kikubwa cha kibinadamu kuliko Am Yisraeli (watu wa Israeli) wengine wote. Sisi vilevile tunahitaji kuheshimu nyadhifa za marabbi wetu, wachungaji na mapadri, lakini nyadhifa zao hakika haziwatengi wao na ubinadamu pamoja na udhaifu wake, kama vile washarika wengine wote wanavyoupitia.

Hii inatuleta katika somo la Miriam (Maria) mama wa Yeshua.

Uri (Luka) {1:48} Kwa kuwa Amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mwenye hali ya chini. Hivyo tangu sasa vizazi vyote wataniita mbarikiwa.

Ni kweli kwamba HaShem alimpa Miriam nyadhifa iliyobarikiwa na yenye kuinuliwa kati ya wanawake. Walakini hiyo haikumfanya yeye awe zaidi ya wanadamu wengine wote na Andiko linashuhudia hilo.

Uri (Luka) {2:21} Siku nane baadaye, wakati wa kumtahiri mtoto ulipofika, walimpa jina YESHUA, jina ambalo alikuwa amepewa na malaika kabla Hajachukuliwa mimba.{2:22} Siku zilipotimia za Miriam kutakaswa kama walivyotakiwa na Sheria ya Moshe (Mose), wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerushalyim (Yerusalemu) ili Wamweke mbele ya BWANA; {2:23} (Katika Sheria ya Bwana imeandikwa: "Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume atawekwa wakfu kwa Bwana;"){2:24} Na walikwenda ili watoe sadaka: hua wawili au makinda wawili ya njiwa, kama ilivyotakiwa katika Sheria ya BWANA.

Kwa kiwango ambacho Miriam alibarikiwa hakikumfanya yeye atengwe kutozifanya mitzvot (amri) za Torati. Mwanamke anahesabiwa kuwa na unajisi wa kiibada siku thelathini na tatu baada ya kumzaa mtoto wa kiume.Huu ndiyo ukweli uliokuwepo kuhusu Miriam japo kuwa mwanae alikuwa ni Yeshua, Mwana wa M-ngu.

Vayikra / Walawi {12:2} Waambie bnei Yisrael (wana wa Israeli) hivi: Mwanamke akipata mimba, akajifungua mtoto wa kiume, atakuwa najisi kwa muda wa siku saba kulingana na siku zake zihusikanazo na hali ya wanawake. {12:3} Mtoto huyo atatahiriwa govi lake katika siku yake ya nane. {12:4} Kisha mama mtoto ataendelea kuwa najisi kwa muda wa siku thelathini na tatu. Wakati huo, kamwe asiguse chochote kilichowekwa wakfu wala kuingia mahali patakatifu mpaka siku za kutakasika kwake zitakapotimia. {12:6} ¡°Siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, iwe amepata mtoto wa kiume au wa kike, atamletea kuhani mlangoni mwa hema la makutano mwanakondoo wa mwaka mmoja kwa ajli ya sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa au hua, kwa ajili ya dhabihu ya dhambi:

Haiwezi kuwa dhahiri ya hivi, kwamba HaShem hana ustahivu na watu zaidi ya ukweli wa kwamba, mama wa Mwana wa M-ngu alikuwa na unajisi wa kiibada na ilimpasa kupitia taratibu zote za utakaso kama zilivyoorodheshwa katika Torati, kabla ya kuingia katika Bet HaMikdash (Hekalu). Hata Yeshua, katika ubinadamu Wake, alikuja kutumikia na siyo kutumikiwa. Andiko liko wazi kabisa kwamba Aliyaendesha maisha Yake yote kwa kuiangalia Torati.

Nafikiri ni jambo jema kwetu sote, bila kujali wadhifa wetu wa kijamii, kidini au kiuchumi, kuweka moyoni yale ambayo tunaonyeshwa hapa katika Parasha Tzav. HaShem hana ustahivu na mtu na sisi sote tunahitaji kutumikiana kwa unyenyekevu. Hakuna hata mmoja wetu ambaye yuko juu ya kutotenda dhambi na sisi sote tunahitaji korban.

Kohellet (Mhubiri) {7:20}"Hakika, hakuna mtu mwadilifu duniani atendaye mema daima bila kutenda dhambi."

Orodha ya masomo ya wiki hii:
*       Kuchangia huduma (Bonyeza Hapa)

YYYYYYYYYYYY
Baruch HaShem
(Jina la BWANA Libarikiwe)
Rabbi Jack (Ya'acov) Farber


Site Design Copyright © 1999- Karl D. Baca All rights Reserved
Congregation Melech Yisrael; 272 Ranee Ave. Toronto, Canada. M6A-1N6 Tel: 416-785-7612 - Fax: 416-785-9414
This site is maintained by the faithful support of its contributors. Donate online; Join our free e-mail group (Here)
A Torah Observant Messianic Jewish יהודים משיחים Congregation, Toronto, Ontario, Canada / Services in Spanish / En Español e Ingles.
An ever changing Messianic Jewish website till King Mashiach Yeshua comes back!!!
אנחנו רוצים משיח עכשיו  / МЫ ХОТИМ МАШИАХА СЕЙЧАС
WE WANT MASHIACH NOW / QUEREMOS AL MASHIAJ YA
יחי אדוננו מורנו ורבינו מלך המשיח לעולם ועד
Moshiach Now

ישוע המשיח