|
CONGREGATION
MELECH YISRAEL OF TORONTO |
||||
|
||||
|
|
|
{8:24} Aliwaleta wana wa Aharon; na Moshe aliweka sehemu ya damu katika incha ya masikio yao ya kulia, na juu ya madole gumba ya mikono yao ya kulia, na juu ya magumba yao ya miguu yao ya kulia: na Moshe alinyunyizia damu kuzungukia juu ya mitzbeach. {8:25} Akachukua mafuta, na mkia wa mafuta, na mafuta yote yaliyokuwapo ndani, na vifuniko vya maini, na mafigo mawili, na mafuta yake, na paja la kulia: {8:26} na kutoka katika kikapu cha mikate isiyo chametz (isiyochachuliwa), iliyokuwepo mbele za HaShem, alichukua keki moja isiyo chametz,na keki moja ya mkate uliotiwa mafuta, na chapati maji,na aliviweka juu ya mafuta, na juu ya paja la kulia: {8:27} na aliviweka vyote juu ya mikono ya Aharon, na mikono ya wanawe, nao wakavipunga mbele ya HaShem dhabihu ya kupunga. {8:28} Moshe alivichukua vyote kutoka katika mikono yao, na alivichoma vyote juu ya mitzbeach juu ya dhabihu ya olah: vilikuwa ni harufu tamu ya kuweka wakfu: ilikuwa ni korban ya kuteketezwa na moto kwa HaShem. {8:29} Moshe alichukua kifua, na alipungia mbele za HaShem dhabihu ya kupunga: ilikuwa ni sehemu ya Moshe’ ya kondoo dume wa wakfu; kama HaShem alivyomuamuru Moshe. Inashangaza, au siyo? Naamini Moshe aliyafanya haya yote kutokana na kumbukumbu yake tu! Labda utasema Moshe aliyaandika yote HaShem alimwelekeza kufanya na kutenda kila jukumu kufuatana na kuangalia maelekezo aliyoandika. Yaani alifuata maelekezo aliyopewa na HaShem pamoja na vielelezo kamili mithili ya vile tunafuata maelekezo ya kampuni katika kuunda fanicha tuliyonunua kama vipande-vipande vya kuunganisha pamoja, sawa? Hapana! Vifungu tulivyokwisha visoma ni baada ya tukio, viko katika nyakati iliyopita. Tunasoma yale ambayo Moshe alikwisha yafanya. Ilikwisha tendeke wakati haya yameandikwa. Je, Moshe aliwezaje kukumbuka yale yote ya kutenda, hasa ukitafakari kipengele kikuu na madhara yaliyofuatia kwa makosa yeyote? Nadhani jibu liko katika ukweli wa kwamba wakati HaShem alimuamuru Moshe, yeye hakulichukulia kiepesi jambo lolote aliloambiwa na HaShem. Kila neno lililotoka mdomoni mwa BWANA, Moshe alijitahidi kujifunza, kukumbuka na kulitimiza kikamilifu. Je, Moshe alikuwa na uweza Fulani usio wa kawaida kukamilisha hili? Kiudhahiri siyo, maana alikuwa ni mtu wa kawaida tu! Wengi wetu tuna matatizo ya kukumbuka amri za HaShem kutoka wakati mmoja hadi mwingine. Je, inamaanisha zinaburuga fikra zetu kutoweza kushika maagizo na masharti haya? Wangapi kati yenu mnayesoma drash (tafsiri) hii mmeajiriwa na kampuni yenye karatasi la muongozo lenye sera na taratibu za kampuni? Je, haikubidi kujifunza hizi sera na taratibu kwa ajili ya utendaji bora wa kazi yako? Je, kuna madhara yeyote iwapo hutafuata kikamilifu hizi sera na taratibu? Je, unanipata ninaelekea wapi? Tutachukua muda kujifunza na kukumbuka sera na taratibu zinazohitajika tulipoajiriwa, lakini ikija kwenye Torati ya HaShem, tunapuuzia mtazamo wote wa kukumbuka amri Zake na hivyo tunapendelea kukubali dhana isiyo sahihi inayosema amri zote zimefutwa na Yeshua. Hakuna haja ya kujifunza au kukumbuka yeyote ile, sawa? Cha kuchekesha ni kwamba hivi sivyo Daudi Melekh Yisrael (Mfalme wa Israeli), mwana zaburi anatuelezea. Yeye alifanya sawa kabisa kama Moshe alifanya na hakika alijihusisha katika kukariri Torati ya HaShem katika maisha yake. Tehillim (Zaburi) {119:1}Wamebarikiwa wasionajisika katika njia, watembeao katika Torati ya HaShem. {119:2} Wamebarikiwa wazishikao shuhuda Zake, na wamtafutao Yeye kwa moyo wao wote. {119:3} Pia hawafanyi maovu: wanatembea katika njia Zake. {119:4} Umetuamuru tushike miongozo Yako kwa bidii. {119:5} Ee kama njia zangu zingeongozwa kushika masharti Yako! {119:6} Ndipo sitaaibika, ninapokuwa na heshema kwa amri Zako zote. {119:7} Nitakusifu Wewe na moyo uliyo na unyofu, nitakapokuwa nimeisha jifunza hukumu Zako ongofu.. {119:8}Nitashika masharti Yako: Ee usiniache mimi mbali. {119:9} Ni kwa vipi kijana ataitakasa njia yake? Kwa kuwa makini kulingana na Neno Lako. {119:10} Kwa moyo wangu wote nimekutafuta Wewe: Ee usiniache ni tangetange mbali na amri Zako. {119:11} Neno lako nimelificha moyoni mwangu, ili nisikutende dhambi. {119:12} Umebarikiwa Wewe, HaShem: nifundishe masharti Yako.Je, umelificha Neno la HaShem moyoni mwako ili usimtende dhambi? Hakika Moshe alifanya, HaMelekh (Mfalme) Daudi alifanya vile-vile, haitupasi nasi tufanya sawa sawa badala ya kinyume chake? YYYYYYYYYYYY |
Site
Design Copyright © 1999- Karl D. Baca All rights
Reserved |