CONGREGATION MELECH YISRAEL OF TORONTO
Kehilat Melech Yisrael, A Messianic Jewish Torah centred Congregation, in Toronto, Canada / קהילת מלך ישראל, קהילה משיחית יהודית שומרת בתורה, הנימצאה בטורונתו, קנדה

פרשות השבוע - Torah Archives

Masomo ya wiki hii

Masomo ya wiki hii

YHome
YMonthly News Letters
YServices & Special Activities
YLocation Map
YWho we Are
YMission Statement
YWhat is Messianic Judaism?
YCMY Academy -Day School
YBooks of Life Catalogue
YRebbetzin Corner
YLinks
..

Y Our E mail
Y Our ICQ Is # 79381635

.

  Jiunge na kundi la email

  

מתשובה למשיח לגאולה במהרה בימינו. זכריה י"ב:י'
ברוך הבא מלך המשיח!

אני מאמין באמונה שלמה בביאת המשיח ואף על פי שיתמהמה עם כל זה אחכה לו בכל יום שיבוא.

ישועה וגאולה אמיתית לכל ישראל.

ČESKÝ | 中文 | DEUTSCH | ENGLISH | ESPAÑOL | FRANÇAIS | עברית |
ITALIANO | KISWAHILI | 한국어 | NEDERLANDS | PORTUGUÊS | РУССКИЙ

פרשת השבוע תולדות

Parashat HaShavua Toldot / Vizazi

Orodha Ya Masomo Ya Wiki Hii:
Y Bereshit / Mwanzo 25:19-28:9
Y Mal'achi / Malaki 1:1-2:7
Y Romim / Warumi 9:6-13
Y Kuchangia Huduma
Y Kutoa Nakala safi

"Onja Ukamilifu WAKE"; Year 5767; Parashat HaShavua Toldot / Vizazi; Bereshit / Mwanzo 25:19-28:9, Mal'achi / Malaki 1:1-2:7, Romim / Warumi 9:6-13; By Messianic Jewish Rabbi Ya'acov Farber, Usharika wa Melech Yisrael, Toronto, Canada;
Shiur / Masomo 5767
5766 Shiur / Masomo

"חווה את מלאותו"

"Onja Ukamilifu WAKE"

"Onja Ukamilifu WAKE"; Year 5767; Parashat HaShavua Toldot / Vizazi; Bereshit / Mwanzo 25:19-28:9, Mal'achi / Malaki 1:1-2:7, Romim / Warumi 9:6-13; By Messianic Jewish Rabbi Ya'acov Farber, Usharika wa Melech Yisrael, Toronto, Canada;
Parashat HaShavua Toldot / Vizazi

Orodha Ya Masomo Ya Wiki Hii:
Y Bereshit / Mwanzo 25:19-28:9
Y Mal'achi / Malaki 1:1-2:7
Y Romim / Warumi 9:6-13
Y Changia Katika Mtandao

Bereshit / Mwanzo {26:25} Akajenga mitzibeakhi (madhabahu) huko, na kuliitia jina la HaShem, na akapiga kambi huko. Huko watumishi wa Yitzikhak wakachimba kisima.

Katika Andiko lote tunaona matamko kama “Liitie jina la BWANA” au “Akaliitia jina la BWANA.” Tunajua kutokana na Andiko, jina ambalo HaShem anataka aitwe ni יהוה. Konsonanti hizi za Kiibrania, zinazosomwa toka kulia kuelekea kushoto, zikiandikwa katika herufi za Kiswahili husomwa kama Yudi Hey Vavu Hey au YHVH. Andiko linasema pia; “Tangaza jina la BWANA,” na “Kupitia jina la BWANA vyote vya duniani vitaokolewa.” Hivyo basi, jina la BWANA linakuwa ni la muhimu sana kwetu. Lakini je, ni lipi jina la BWANA na linatamkwaje? Je, ina maana gani yeyote ile katika lote hili la kuliitia jina la HaShem? Inahusiana na nini?

Kiibrania mada ya M-ngu, kama tuionavyo katika Tanakhi yote (Maandiko ya Kiibrania), ni kuhusu Yule Mmoja atendaye kwa niaba yetu, na Yule Mmoja aingiliaye kati kwa ajili yetu wakati tunataabika. Hivyo wakati HaShem alipomwambia Yitzikhak.

Bereshit {26:2} HaShem akamtokea Yitzikhak na kumwambia, “ Usiende chini Mitzirayim Kaa katika nchi nitakayokuambia. {26:3} Kaa ugenini katika nchi hii, Nami nitakuwa nawe na kukubariki. Nitaimarisha kiapo nilichomwapia Avraham ab’(baba) yako, kwani Nitakupa wewe na uzao wako nchi zote hizi. {26:4} Nitauzidisha uzao wako uwe kama nyota za angani, na nitaupa uzao wako nchi hizi zote. Katika uzao wako goyim wote (mataifa) duniani watabarikiwa, {26:5} kwa sababu Avraham aliitii sauti Yangu, akazingatia maagizo Yangu, mitzivoti(amri) Zangu , masharti Yangu, na toratoti Zangu (mafundisho).”

HaShem anamwambia Yitzikhak katika Maandiko hapo juu, jinsi Atakavyotenda kwa niaba yake na kile Atakachokifanya kwake. Hivyo kutokana na hili na Maandiko mengine katika Torati tunaelewa kwamba, kile ambacho HaShem Anakitaka, ni jina Lake kungáriza kile Akitendacho na/au kile Atakachokifanya. Katika siku ile wakati tukiliitia jina la BWANA, tunakumbuka kile Akitendacho katika maisha yetu na ulimwenguni, pamoja na yale Aliyokwisha kuyatenda. Kwa maneno mengine jina la HaShem linangárizia tabia Yake; jina Lake ni kile Alichokifanya na kile Atakachokitenda. Hata hivyo, jina Lake kama tujuavyo leo, si jina kama linavyotamkwa.

Sasa kama nilivyosema, kuna huu msisitizo unaoendelea katika Andiko juu ya kulitangaza jina la BWANA, hebu tuangalie mfano mmoja.

Yeshiyahu / Isaya {43:10} HaShem akasema hivi, “Nyinyi Waisraeli ni mashahidi wangu; niliwachagua muwe watumishi Wangu, mpate kunijua na kuniamini, kwamba Ndimi peke Yangu M-ngu: kabla Yangu hajapata kuwepo mungu mwingine, wala hatakuwepo mungu mwingine.. {43:11} Mimi peke Yangu Ndimi Hashem hakuna mkombozi mwingine ila Mimi. {43:12} Nilitangaza, na Niliokoa, na Nilionyesha, wakati hakuwepo M-ngu yeyote wa kigeni kati yenu: kwa hiyo nyinyi ni mashahidi Wangu, asema HaShem kwamba Mimi ni M-ngu.”

Hebu angalia yaliyopo hapa! Jina la BWANA linaunganishwa na yale Aliyoyatenda. Amejifunua Yeye Mwenyewe: Amewaokoa, Amewakomboa, hakuna kama Yeye, na hakuna mkombozi mwingine mbali na Yeye. Sasa swali ni hili. Kama jina la BWANA ni la muhimu sana, kwa nini tusilitumie jina Lake? Kusema kweli katika mapokeo ya Kiyahudi unakatazwa kulitamka jina la BWANA. Bali anaitwa HaShem ikimaanisha “Jina.” Hatutumii wala kutamka YHVH sana kwa sababu, hakuna ajuaye hakika jinsi ya kulitamka au lina maana gani. Wengi wameongezea herufi tamfu kwenye YHVH ambazo hazikuwepo katika hata moja ya maandishi ya Kibiblia ya hapo awali. Wafasiri wa Biblia kama vile ‘King James Version’, wameongezea herufi tamfu, na huu ni ukisiaji mtupu – kazi ya mafikara ya kibinadamu. Baadhi ya tafsiri zinatamka Y kama J, nayo pia ni kosa.

Jina katika Andiko halimtambulishi tu mtu, bali jina lao linatuambia pia jinsi watakavyokuwa pamoja na yale watakayoyatenda. Hivyo Yeshua aliitwa Wokovu. Ndiyo, ni M-ngu ajaye duniani kama mtu, lakini cha muhimu ni kwamba jina Alilopewa, katika mwili, linaambatana na kile Atakachokifanya mbeleni. Kama vile jina la HaShem katika Shemot(Kutoka), “YHVH” linahusiana na kile Anaenda kukitenda kwa Yisraeli (Israeli), k.v. kuwakomboa kutoka Mitzirayim(Misri). Ukweli uleule unashikilia hapa katika Parasha yetu; jina Lake linashikamana na kile Anaenda kukitenda kwa Yitzikhak.

Yeshua sasa ni Jina lililo juu ya Majina yote. Hivyo siyo shani kwamba jina la M-ngu, YHVH, haliongelewi tena au hata kujulikana sasa! Hii ndiyo sababu halikutajwa kabisa katika Brit Chadasha (Agano Lililohuishwa). Naamini HaShem alifanya hivyo ili kwamba jina la Yeshua litakuwa ni Jina jipya, Jina ambalo litatamka kile ambacho HaShem alikuwa Anaenda kukitenda kuanzia wakati ule na kuendelea. Kwa hiyo, YHVH limefunuliwa kikamilifu katika Jina la Yeshua. Ukamilifu wa tabia Yake, ukamilifu wa uweza Wake na ukamilifu wa matendo Yake yote yamekuja kuelezewa, kufunuliwa na kueleweka kupitia maisha pamoja na Jina la Yeshua. Hili ni Jina HaShem anatutaka tuje Kwake nalo, na hili ni Jina Analotutaka tulijue. Ndiyo bado tunarejea kwa HaShem kama M-ngu Baba na bado tunaomba kwa M-ngu Baba, lakini ni kwa kupitia Jina la Yeshua, kwa sababu hilo ndilo linatupa haki kuja katika uwepo wa HaShem. Utamkaji wa YHVH haujulikani kwetu na hauwezi tena kutamkwa kwa sababu jina la Yeshua limetupa sisi ufunuo mpya wa nani ni YHVH na ni kipi Anakitenda kwa ajili yetu SASA.

Kama unataka kujua ukamilifu wa M-ngu, kama unataka kushuhudia ukamilifu wa uweza Wake, na kama unataka dhambi zako sisamehewe, huu ni wakati wa kumjua Yeshua. Yeye ni ufunuo mkamilifu wa M-ngu; Yeye ni ufunuo mkamilifu wa YHVH.

YYYYYYYYYYYY
Baruch HaShem
(Jina la BWANA Libarikiwe)
Rabbi Ya'acov Farber

Site Design Copyright © 1999- Congregation Melech Yisrael All rights Reserved
Congregation Melech Yisrael; 272 Ranee Ave. Toronto, Canada. M6A-1N6 Tel: 416-785-7612 - Fax: 416-785-9414
This site is maintained by the faithful support of its contributors. Donate online; Join our free e-mail group (Here)
A Torah centred Messianic Jewish יהודים משיחים Congregation, Toronto, Ontario, Canada / Services in Spanish / En Español e Ingles.
An ever changing Messianic Jewish website till King Mashiach Yeshua comes back!!!
אנחנו רוצים משיח עכשיו  / МЫ ХОТИМ МАШИАХА СЕЙЧАС
WE WANT MASHIACH NOW / QUEREMOS AL MASHIAJ YA
יחי אדוננו מורנו ורבינו מלך המשיח לעולם ועד
Moshiach Now

ישוע המשיח