CONGREGATION MELECH YISRAEL OF TORONTO
Usharika wa Melech Yisrael, Toronto, Canada - Kehilat Melech Yisrael, A Messianic Jewish Torah centred Congregation, in Toronto, Canada / קהילת מלך ישראל, קהילה משיחית יהודית שומרת בתורה, הנימצאה בטורונתו, קנדה

פרשות השבוע - Parashot HaShavua

 Masomo ya Biblia Kwenye Mtandao

ENGLISH / ESPAÑOL / PORTUGUÊS / ITALIANO / FRANÇAIS / MAGYAR / KISWAHILI / / 한국어 / РУССКИЙ / עברית

Masomo ya wiki hii

YHome
YMonthly News Letters
YServices & Special Activities
YLocation Map
YWho we Are
YMission Statement
YWhat is Messianic Judaism?
YCMY Academy Day School
YBooks of Life Catalogue
YRebbetzin Corner
YLinks
..

Y Our E mail
Y Our ICQ Is # 79381635

.

  Jiunge na kundi la email
  

Masihi Myahudi

* DO WE WANT MASHIACH NOW?
FALSE MESSIAHS - TRUE MESSIAH
DO YOU WANT MASHIACH NOW?

UNTIL MASHIACH RETURNS

מתשובה למשיח לגאולה במהרה בימינו. זכריה י"ב:י'
ברוך הבא מלך המשיח!

אני מאמין באמונה שלמה בביאת המשיח ואף על פי שיתמהמה עם כל זה אחכה לו בכל יום שיבוא.

Radio Melech HaMashiach - רדיו מלך המשיח; a Messianic Jewish Radio Station on the Internet.

ישועה וגאולה אמיתית לכל ישראל.

פרשת השבוע משפטים
Parashat Mishpatim / Maamuzi

Y Shemot / Kutoka 21:1-24:18
Y Shemot / Kutoka 30:11-30:16
Y Melachim bet / 2 Wafalme 12:1-12:17
Y Mattityahu / Matayo 5:38-42
Y Kuwasha Mishumaa 5:40 p.m.
Y Mwisho wa Shabati 6:51 p.m.
Y
Kutoa Nakala safi (Bonyeza)
Y Rosh HaChodesh "Adar"
Y Kuchangia huduma (Bonyeza)

“Hakuna kitakatifu isipokuwa HaShem” פרשת השבוע משפטים / Prashati HaShavua Mishpatim / Maamuzi; Usharika wa Melech Yisrael, Toronto, Canada
Shiur 5766
5765 Masomo ya Biblia

“Hakuna kitakatifu isipokuwa HaShem”

Shemot / Kutoka {24:15} Basi, Moshe (Mose) akaenda mlimani, na wingu likaufunika mlima. {24:16} Shekinah (uwepo wa kuonekana) ya HaShem ikatua juu ya Hari (Mlima) Sinai na wingu likaufunika mlima kwa muda wa siku sita. Siku ya saba M-ngu akamwita Moshe kutoka katikati ya lile wingu. {24:17} Shekinah ya HaShem alionekana mbele ya macho ya Bnei Yisraeli (wana wa Israeli) kama moto unaowaka juu ya mlima. {24:18} Moshe akaingia ndani ya lile wingu, akapanda mlimani; na Moshe alikuwa juu mlimani siku za machana arobaini na usiku arobaini.

Kokote uendapo Yisraeli (Israeli) siku hizi, utakuta ziara iliyojengwa katika sehemu maalumu takatifu: kanisa lililojengwa mahala ambapo labda Yeshua alifanya hiki au Miriam (Maria mama yake Yeshua) alifanya kile; kanisa ambalo Shauli (Paulo) alikuwepo, au nyumba alimoishi Kefa (Petro), na sehemu hizi zote zinatazamwa kama takatifu. Kwa hiyo ukizitembelea sehemu hizi unatarajiwa kuingia kiuchaji na ukiwa umevaa kiheshima. Wanaume hawawezi kuingia wakiwa wamevaa kaptura: wanawake wanahitaji kuvaa nguo zinazofunika magoti na mabega yao na katika maswala mengine, wafunike vichwa vyao. Kuna hata ziara ambayo mlango wake umejengwa mfupi sana ili kwamba wote waingiao wanalazimika kuinama ili kupita.

Kuna Bustani ya Gethsemane, Kanisa la Mateso (Agony), Chumba cha Karamu ya Mwisho (Last Supper), 'Dormition Abbey', Kanisa la Kaburi Takatifu 'Holy Sepulchre', Kanisa la 'Nativity' (Alipozaliwa Bwana) na zaidi na zaidi, na bado hatujatoka sana eneo la Yerushalayim (Yerusalemu). Kweli tumebarikiwa kwamba hakuna ajuaye wapi ni Hari Sinai, kwa sababu kama ingalijulikana, hakika sasa kungalikuwa na aina fulani ya ziara, hekalu au kanisa lililokwisha jengwa juu yake, na kudaiwa kuwa ni takatifu, wakati huohuo wakitoza kiingilio. Cha kusikitisha ni kwamba kuna mlima Mitzrayim (Misri) ambao unadhaniwa kuwa ni Hari Sinai, ambao una kanisa chini yake.

Hakika ingawa HaShem alikuwapo juu ya Hari Sinai, kama inavyoelezewa katika Parasha yetu ya wiki hii, na kwamba mlima ulikuwa mtakatifu na hukana yeyote aliweza kuusogelea bila ya kibali cha HaShem na maelekezo ya ufasaha ya jinsi ya kufanya hivyo. Bnei Yisraeli hawakuruhusiwa kuusogelea mlima hivihivi tu, bado walihitajika kupitia tevilah (kuzamishwa), ili kwamba wawe wasafi kiibada na kuweza kuusogelea. Ukweli ni kwamba kizuizi kiliwekwa ili kuwazuia.

Wanyama walizuiwa kujiendea sehemu yeyote karibu na mlima, na kutokutii kokote kwa aidha mwanadamu au mnyama kulimaanisha kifo hakika. Aharoni na wale walioambatana naye waliruhusiwa tu nusu ya njia kufikia juu milmani, wakati Moshe peke yake, mtu mmoja kati ya wanaume zaidi ya laki sita, aliruhusiwa kupanda hadi juu.

Inachekesha kwamba hakuna hata neno moja katika Andiko linalomkataza yeyote asizurure Hari Sinai baada ya Shekinah ya HaShem kuondoka milmani, na tunaona bnei Yisraeli wakihama kambi kuelekea sehemu nyingine baada ya hapo. Unaweza kuwa na uhakika kwamba wanyama walianza kuwa malishoni kwenye miteremko yake na wachungaji wahamaji walikuwa wakizurura kwa uhuru tena juu yake pamoja na mifugo yao. Unaona, hakuna kitu chochote kitakatifu na mlima, ulikuwa ni mlima tu! Muda tu ambao Hari Sinai ulikuwa mtakatifu, ni wakati HaShem alikuwapo pale. Zaidi ya hapo ulikuwa ni mlima tu, na bado ni mlima tu popote utakapokuwa! Maana siyo mlima ambao ni mtakatifu bali ni HaShem.

Siku hizi watu wengi wanafanya rabsha kubwa kuhusiana na 'Temple Mount' (Mlima wa Hekalu). Kuna tangazo kubwa katika lango la Mlima, mara ukitoka Kotel HaMaaravi (Ukuta wa Magaharibi), ambao unamwaonya yeyote aliye Myahudi asipande juu ya Mlima, asije kwa makosa akakanyaga katika ardhi ambayo ilishikilia Kadosh HaKodashim (Patakatifu pa Patakatifu).

Sasa sitaki kuwa mtu asiye mstahivu na wala siyo nia yangu kukebehi; walakini, hakuna kitu chochote kitakatifu, hakuna uwakfu wowote kuhusiana na 'Temple Mount', kama Bet HaMikdash (Hekalu) halipo pale na zaidi kama uwepo wa HaShem hauko, yaani Shekinah Yake haiko ndani ya Bet HaMikdash. Mezuzah (kiboksi kidogo juu ya nguzo ya mlango wa nyumba), siyo takatifu tu kwa sababu kina kigombo chenye kisehemu cha Torati iliyoandikwa kwa mkono; Biblia siyo takatifu kwa sababu tu ina Neno la M-ngu; hakuna kitu kinachoitwa mafuta matakatifu ya upako au maji matakatifu, kama hakuna Bet HaMikdash pamoja na uwepo wa Shekinah wa kunyunyizia juu yake.Hebu tukubaliane na ukweli; hakuna kitakatifu isipokuwa HaShem. Sehemu zinakuwa takatifu tu kama Uwepo wa Kimungu uko pale na vitu vinakuwa vitakatifu kama vinatumika kuhudumu uwepo Wake. Au sivyo ni vitu tu na ni sehemu tu, yaani wino na karatasi tu.

Wakati Melekhi (Mfalme) Yeshua HaMashiakhi anarudi, Atalijenga Bet HaMikdash na kufanya maskani yake pale, na utakatifu wa hapo awali wa Bet HaMikdash utarejeshwa kwa Yisraeli na ulimwenguni.

Yeshayahu (Isaya) 66:23 - "Katika kila sikuku ya mwezi mpya (kuanzia mwezi mmoja wa Kiibrania hadi mwingine), na katika kila siku ya Shabbati (Sabato), binadamu wote watakuja kuniabudu", asema HaShem.

YYYYYYYYYYYY
Baruch HaShem
(Jina la BWANA Libarikiwe)
Rabbi Ya'acov Farber


Site Design Copyright © 1999- Congregation Melech Yisrael All rights Reserved
Congregation Melech Yisrael; 272 Ranee Ave. Toronto, Canada. M6A-1N6 Tel: 416-785-7612 - Fax: 416-785-9414
This site is maintained by the faithful support of its contributors. Donate online; Join our free e-mail group (Here)
A Torah centred Messianic Jewish יהודים משיחים Congregation, Toronto, Ontario, Canada / Services in Spanish / En Español e Ingles.
An ever changing Messianic Jewish website till King Mashiach Yeshua comes back!!!
אנחנו רוצים משיח עכשיו  / МЫ ХОТИМ МАШИАХА СЕЙЧАС
WE WANT MASHIACH NOW / QUEREMOS AL MASHIAJ YA
יחי אדוננו מורנו ורבינו מלך המשיח לעולם ועד
Moshiach Now

ישוע המשיח